Unknown Unknown Author
Title: Babu Tale afikishwa Mahakamani, atakiwa kujieleza ni kwanini asifungwe
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa mwanamuziki wa Diamond Platnumz na Tip Top Connection, Hamis Tale Tale ‘Babu Tale’ Jumanne hii alishikwa na polisi na kufikishwa M...
Meneja wa mwanamuziki wa Diamond Platnumz na Tip Top Connection, Hamis Tale Tale ‘Babu Tale’ Jumanne hii alishikwa na polisi na kufikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Babu Tale alitakiwa kueleza mahakama ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.
Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.
Wiki kadhaa zilizopita, Bongo5 ilizungumza na Tale ambaye amedai kuwa makubaliano hayo yalifanywa baina ya sheikh huyo na marehemu kaka yake, Abdu Bonge na kwamba yeye hahusiki.
“Mimi na marehemu brother yangu tulifungua kampuni ya Tip Top Connection pamoja, mimi nifanye muziki yeye anisaidie.. Alipoona nimesogea akaona aachane na mimi ili afanye movie. Kwahiyo hakuwa anajua mimi ninachokifanya kwenye muziki, mimi pia sikuwa najua anachokifanya kwenye movie, imeenda akawa anafanya movie, sijawahi hata kushiriki hata kwa njia ya kuonekana location, hata kukaa nao kuongea nao lolote au kusainisha nao mkataba, so I know nothing,” amesema Tale.
“Mwaka juzi wakati nipo Uingereza yule Mzee akasikika kwenye U Heard kwamba anaidai Tip Top Connection milioni 50. Soudy Brown alimhoji akamuambia unamjua Babutale, akasema namjua lakini sijawahi kuongea naye hata siku moja. Akapeleka kesi mahakamani wakati brother yupo hai baadaye akaja akawa amefariki mimi nikawa sijui tena kinachoendelea. Kumbe yule mwanasheria alikuwa na marehemu brother na yule mzee wanakutana mahakamani. Mwaka huu kama mwezi mmoja uliopita akanipigia mtu simu, simu yangu napigiwa na watu wengi sana hii ‘mimi mwanasheria, unashtakiwa kwa kosa la kumdhulumu mtu kazi.’ Nikamuambia hizi kazi alikuwa akisimamia marehemu brother yangu kwahiyo story unazoniletea mimi unanirusha roho. Nikamwambia mimi naishi maisha yangu sijui kinachoendelea na sijawahi kujihusisha na chochote na hata huyo sheikh kama ana sehemu yoyote ambayo ameona kuna jina langu nimesaini naye niko tayari hata akisema ananidai,” alisisitiza.
“Kwahiyo wakati wanazunguka na kesi yao wakapita Brela kuchunguza hii kampuni wako nani na nani? Wakagundua kuna marehemu Abdul Bonge, mimi hapa na brother yangu mwingine lakini hawajui labda kwamba sisi tuligawana kila mtu na majukumu yake kwasababu kila mmoja alikuwa anafanya kile ambacho anakiweza.”
“Kwahiyo wameenda mahakamani wamepata barua wanikamate kwasababu mimi ninadaiwa. Mimi niko nyumbani wamekuja kugonga nyumbani kwangu kama majambazi. I was like wewe unakuja unajua hapa kwa nani? Mbona unataka kuniharrass rafiki yangu? Wewe unakuja kumkamata mtu usiyemfahamu! ‘Wewe si Tale’ walikuwa hawajui kama mimi ndio Babutale. Kama wao wananitaka wangeniambia mimi nipo Oysterbay polisi hapa, hawajaja. Mimi asubuhi ndio nikatoka nikaenda kumfuaya yule mwanasheria ambaye anasimamia kesi kuaniambia kuna nini naona kama watu wananitumia meseji kwamba nimeshtakiwa, akanihadithia in and out.”
“Tangu nijue kila kitu leo nina siku ya nne, I know nothing, sijawahi kumuona huyo mzee hata akitokezea sehemu simjui kwa sura. Lakini sasa yule mwanasheria wa yule mzee anasema Babutale ana hela, tukimshtaki Babutale atauza nyumba au watu watamchukua au tukimdhalilisha kwenye mitandao ataona aibu atataka kulipa. Vaa kiatu changu, wewe ni sehemu gani unalipa hapo? Sijui chochote, lakini wao wanaamini kwasababu mahakama imewaamuru nimewalipe milioni 250 na wanaamini mimi nina hela basi nitawalipa tu, haiwezekani,” amesema Tale
Credit: Habari hii imetumia sehemu ya habari iliyoandikwa na gazeti la mwananchi.

Advertisement

Post a Comment

 
Top