Unknown Unknown Author
Title: Shetta adai msanii kufanya muziki bila kuwa na management ni ‘uswahili’
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki Shetta amefunguka na kueleza faida alizozipata baada ya kutangaza management yake mpya ambayo imemsaidia kufanya mambo amba...
Msanii wa muziki Shetta amefunguka na kueleza faida alizozipata baada ya kutangaza management yake mpya ambayo imemsaidia kufanya mambo ambalimbali ambayo hapo awali alikuwa akiyafanya mwenyewe.
Akiongea na tygatattoo Jumapili hii, Shetta amesema ameamua kufanya muziki wake ‘kiprofessional’ zaidi tofauti na awali.
“Kuamua kuwa na management ni kuamua kuwa professional, huwezi kuwa msanii huna management, huna mtu ambaye anakupangia ratiba, huna mtu ambaye nasimamia kazi zako, huyo ni uswahili,” alisema Shetta.
Aliongeza, “Ni kitu kizuri lazima uwe professional, yaani haiwezekani mtu akaja akadeal na mimi direct, lazima awasiliane na uongozi, mimi napewa tu taarifa ya mikakati na nini kifanyike,”
Pia rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Namjua’ amewataka mashabiki wa muziki wake kusubiria surprise za kazi mpya.

Advertisement

Post a Comment

 
Top