Ukitaja watangazaji wa redio wenye mashabiki wengi na wanaosikilizwa zaidi kwenye redio za Tanzania hutoacha kumtaja Diva The Bawse.
Akiwa na mtaji wa zaidi ya followers milioni moja kwenye Instagram, staa huyo amekifanya kipindi chake, Ala za Roho kuwa moja ya vipindi muhimu vya Clouds FM. Hivi karibuni ameendelea kukiboresha zaidi na kuongeza mahojiano na mastaa wa nje ya Tanzania.
Miongoni mwa mastaa aliowahi kuwahoji siku za nyuma kwenye show yake ni Iyanya, Tekno na Seyi Shay wa Nigeria – kutaja wachache tu.
Na sasa mtangazaji huyo ametupeleka kwenye ulimwengu wake wa uandaaji wa interview za aina hiyo kwaajili ya kipindi chake.
“It takes me hours before international interview,”
“Yaani ninaandika mails very proffessional, then napiga simu to set everything on. Nafanya research kama huyu in case nikifanya naye atakuwa na impact or niamue mwenyewe to just mtengeneza mtu kwa Tanzania awe mkubwa and thank me later,” anasema.
“In short I work my ass off, likijaga suala la show yangu huwa I am not playing. I will encourage some radio personalities wawe very creative and dedicate time yao kwenye kazi yao and respect the fanbase na sio kuwaletea pozi mashabiki.
Mashabiki is everything in life, I listen to a lot music to make sure I give the best to the listeners. Interview za ndani na nje zinakuwa exclusive hasa, sio kazi rahisi, ndio maana I am not just a radio or media personality, I am Super brand! It takes years to be one, dedication is the key, kupenda kazi yako unayofanya is the key to success.”
Pamoja na utangazaji staa huyo amekuwa na shughuli zingine kibao za kumuingizia mkwanja town.
“Depending on the working schedule and availability, I accept a part time work on and deal with my company called Dream Futures to make more millions to survive. Guess I ain’t got free time because I am more focused on different opportunities that help me become successful in life and must admit numbers don’t lie, working hard pays man.”
Post a Comment