Unknown Unknown Author
Title: Exclusive Video: Zamaradi azungumzia sakata la show yake ya Take One kupewa adhabu na TCRA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Zamaradi Mketema alijikuta kwenye kitimoto wiki kadhaa zilizopita baada ya kipindi chake cha Take One cha Clouds TV, kumhoji shoga na kupele...
Zamaradi Mketema alijikuta kwenye kitimoto wiki kadhaa zilizopita baada ya kipindi chake cha Take One cha Clouds TV, kumhoji shoga na kupelekea malalamiko makubwa kiasi cha kuifanya mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA kukipa adhabu kituo hicho cha runinga.

Nilikutana naye wiki hii na kumuuliza alikuwa katika hali gani kipindi hicho.
Amedai kuwa tofauti na matarajio ya wengi, hicho hakikuwa kipindi kigumu bali cha ushindi kwakuwa aliweza kufichua mambo mengi ambayo hadi serikali iliamua kuyachukulia hatua kuhusiana na vitendo vya ushoga nchini.
Amesema aliona jambo ambalo wengi wanaogopa kulisema lakini linahitaji kudhibitiwa na hivyo alifanya kipindi hicho akitegemea mrejesho hasi lakini lengo lake likiwa chanya.
“Kitu ambacho kilinifurahisha ni kuwa serikali ilianza kutake action baada ya hicho kipindi, siku zote walikuwa wapi? kwahiyo ina maana kilikuwa na positive impact kwa upande wangu mimi,” alisema.
Amesema kipindi chake kimesaidia kuamsha mambo ya siri yatakayoisaidia serikali kupambana vyema na tatizo la ushoga. Mtazamae Zamaradi hapo chini akifunguka kuhusiana na sakata hilo.

Advertisement

Post a Comment

 
Top