Unknown Unknown Author
Title: JB kuacha kuigiza, adai ataachia filamu moja ya mwisho
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Msanii mkongwe wa filamu Jacob Stephan ‘JB’ amefunguka kwa kusema kuwa ataachia filamu yake moja ya mwisho na baada ya hapo atawaachia vijan...
Msanii mkongwe wa filamu Jacob Stephan ‘JB’ amefunguka kwa kusema kuwa ataachia filamu yake moja ya mwisho na baada ya hapo atawaachia vijana fani hiyo.
Muigizaji huyo ambaye yupo mbioni kuachia filamu yake mpya ‘Kalambati Lobo’, amesema baada ya filamu hiyo ataachia filamu moja na mwisho na baada ya hapo atapumzika.
“Nimekuwa nikipokea simu nyingi na meseji kutoka kwa wapenzi wangu kwa nini napunguza kutoa filamu, jamani naomba niwaambie ukweli najiandaa kupumzika kuigiza,” aliandika JB kupitia instagram yake. “Lakini najitengeneza kuwa producer mkubwa zaidi ndiyo maana natengeneza hata tamthilia,”
Aliongeza, Nimeigiza tangu 1998 hadi sasa, nakaribia umri wa miaka 50, kwa umri wangu natakiwa niwekeze zaidi kwa vijana ambao naamini wanaweza kufanya vizuri zaidi. Kwa hiyo baada ya filamu ya ‘Kalambati Lobo’ nitafanya movie yangu moja ya mwisho na baada ya hapo kazi itakayobaki ni kuwasaidia vijana kupitia Jerusalem Film. Nawapenda sana na asanteni sana kwa kuniunga mkono, hamjawahi kuniangusha, nawapenda sana,”
Muigizaji huyo amewai kufanya vizuri na filamu kama, Danija, DJ Ben, Bonge la Bwana, Mzee wa Swagga pamoja na Jacob stephene,”

Advertisement

Post a Comment

 
Top