Unknown Unknown Author
Title: P-Funk aeleza sababu ya kutokuwa na mpango wa kuwarudisha wakongwe waliopotea
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Producer mkongwe wa Bongo Flava, P-Funk Majani, amesema hana mpango wa kuanza kuwarudisha wasanii wakongwe aliofanya nao kazi miaka ya nyum...
Producer mkongwe wa Bongo Flava, P-Funk Majani, amesema hana mpango wa kuanza kuwarudisha wasanii wakongwe aliofanya nao kazi miaka ya nyuma kwasababu anaamini ni lazima asonge mbele kusaidia vipaji vipya.
Amedai kuwa ili producer aweze kudumu kwa miaka mingi ni lazima awe na uwezo wa kubadilisha kazi zake na hata wasanii wa kufanya nao kazi.
“Kwangu mimi kuweza kupiga hatua kusonga mbele inabidi usirudi nyuma. Kusonga mbele inamaanisha tafuta vijana chipukizi, sauti zingine, talent zingine, zijenge, ziunde zile,” Majani ameiambia tygatattoo.
Amedai kuwa amechukua mfano wa role model wake, Dr Dre ambaye anadai alianza kufanya kazi na NWA na Snoop Dogg kabla ya kuwatoa Eminem, baadaye 50 Cent na kisha Kendrick Lamar.
“You have to move, producer maisha yake yanaweza kuwa marefu mno kwenye industry lakini lazima abadilishe vipaji,” amesisitiza.

Advertisement

Post a Comment

 
Top