Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, staa huyo alikataa kuchukua dola milioni 5 alizopewa ili atumbuize kwenye show ya chama cha Republican wakati wa mkutano wake wa hivi karibuni huko Cleveland, Marekani.
Vyanzo vimedai kuwa mchezaji wa kikapu, LeBron James pamoja na meneja wa Bieber, Scooter Braun ni watu waliomshawishi aikatae ofa hiyo.
James alimkataza Bieber kutumbuiza huku Braun akimtishia kujiondoa kama meneja wake iwapo angekubali.
CAA, kampuni inayomwakilisha Bieber, ilipokea ofa hiyo. Ilikuwa ni ya kutumbuiza kwa dakika 45 kwenye ukumbi karibu na Quicken Loans Arena, ambako mkutano mkuu wa Republican ulifanyika.
Japo mapromota hao walidai kuwa show hiyo haikuwa ya kisiasa, kiasi hicho cha fedha kilichangwa na wadhamini wa chama hicho.
Kiasi hicho cha fedha kingekuwa malipo makubwa zaidi ya mara moja kwa Bieber kupewa katika maisha yake ya muziki, au kikubwa zaidi kwa msanii kuwahi kupewa mara moja.
Awali Bieber alikuwa amefikiria kutumbuiza kutokana na kuwa na asili na Canada na kwamba siasa ya Marekani haimhusu.
Hata hivyo meneja wake ni shabiki mkubwa wa mgombea Urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton na pia mmoja wa wachangishaji fedha.
Inasemekana kuwa awali Braun alishauri Bieber atumbuize huku kukiwa na mabango yaliyoandikwa ‘Black Lives Matter’ kwenye show hiyo.
Mapromota hao walikaa wazo hilo na kupendekeza mabango yaandikwe ‘All Lives Matter.’ Mapromota hao pia walimkataza Bieber asiseme kitu chochote kibaya kumhusu Trump au chama chake. Matokeo yake, Braun alisema asingemwakilisha tena Bieber kama angechukua ofa hiyo.
Ingawa mapromota walimweleza Scooter kuwa LeBron James angekuwepo kwenye tukio hilo huko Cleveland wiki hiyo kuwakaribisha wanasiasa bila kuwa na msimamo wa kisiasa, James alidaiwa kukataa na kumtaka Bieber naye aitose ofa hiyo.
Bendi ya Bieber pia ilikuwa na ushawishi na uamuzi wake. Kwa mujibu wa ripoti, kila member wa bendi hiyo ni mweusi na kila mmoja aliipinga show hiyo.
Mwishowe, Bieber akawa hana ujanja zaidi ya kuikataa ofa hiyo.
Mwishowe, Bieber akawa hana ujanja zaidi ya kuikataa ofa hiyo.
Post a Comment